Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Lucas559/Ugonjwa wa kidonda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lucas559/Ugonjwa wa kidonda
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuGastroenterology
DaliliMaumivu ya tumbo, kuhara kulikochanganyika na damu, kupungua uzito, homa, upungufu wa damu[1]
Miaka ya kawaida inapoanzaMiaka 15–30 au zaidi ya miaka 60[1]
MudaMuda mrefu[1]
VisababishiHavijulikani[1]
Njia ya kuitambua hali hiikolonoskopia kwa kutumia biopsi ya tishu[1]
Utambuzi tofautiDysentery, Ugonjwa wa Crohn, ischemic colitis[2]
MatibabuKubadilisha lishe, dawa, upasuaji[1]
DawaSulfasalazine, mesalazine, steroids, immunosuppressants kama vile azathioprine, biological therapy[1]
Idadi ya utokeaji wakeHadi watu 5 kwa kila watu 1000 people[3]
Vifo47,400 pamoja na ugonjwa wa Crohn (2015)[4]

Ugonjwa wa vidonda vya utumbo mkubwa ( UC ) ni hali ya muda mrefu ambayo husababisha kuvimba na vidonda kwenye utumbo mkubwa na rektamu . [1] [5] Dalili kuu za ugonjwa unaoendelea ni maumivu ya tumbo na kuhara kulikochanganyika na damu . [1] Kupungua uzito, homa, na upungufu wa damu pia ni dalili. [1] Mara nyingi, dalili huja polepole na zinaweza kuwa ndogo au kubwa. [1] Dalili kwa kawaida huja na kupotea. [1] Matatizo yanaweza kujumuisha kupanuka kwa utumbo mkubwa, kuvimba kwa jicho, viungo, au ini na saratani ya utumbo mkubwa. [1] [6]

Sababu ya UC haijulikani. [1] Nadharia zinahusisha kutofanya kazi kwa mfumo wa kinga, jeni, mabadiliko ya bakteria ya kawaida ya utumbo na mambo ya mazingira. [1] [7] Viwango vya ugonjwa huu vinaonekana kuongezeka kwenye ulimwengu uliostawi huku wengine wakipendekeza kuwa ni matokeo ya kuathiriwa kwa kiwango cha chini na maambukizo ya utumbo, au kwa lishe na mtindo wa maisha wa Magharibi . [5] [8] Kuondolewa kwa kifuko katika umri mdogo kunaweza kuwa kinga. [8] Utambuzi kwa kawaida hufanywa kupitia kolonoskopia na biopsi ya tishu . [1] Ni aina ya ugonjwa wa uchochezi wa matumbo (IBD) pamoja na ugonjwa wa Crohn na uvimbe mdogo wa utumbo mkubwa. [1]

Mabadiliko ya lishe, kama vile kuendelea kukula lishe yenye kalori nyingi au lishe isiyo na laktosi, yanaweza kuboresha dalili. [1] Dawa kadhaa hutumiwa kutibu dalili na kupunguza maumivu, ikiwa ni pamoja na aminosalicylates kama vile mesalazine au sulfasalazine, steroids, immunosuppressants kama vile azathioprine na biopic therapy. [1] Kuondolewa kwa koloni kupitia upasuaji kunaweza kuwa muhimu ikiwa ugonjwa umekithiri, haukubali matibabu, au ikiwa matatizo kama vile saratani ya koloni yanatokea. [1] Kutolewa kwa utumbo mkubwa na rektamu kwa ujumla huponya hali hiyo. [1] [8]

Pamoja na ugonjwa wa Crohn, takriban watu milioni 11.2 waliathiriwa kufikia 2015. [9] Kila mwaka, mtu 1 hadi 20 kwa kila watu 100,000 na watu 5 hadi 500 kwa kila watu 100,000 huathiriwa. [5] [8] Ugonjwa huu unaripotiwa zaidi katika Amerika ya Kaskazini na Ulaya kuliko maeneo mengine. [8] Mara nyingi huanza kwa watu wenye umri wa miaka 15 hadi 30, au walio na zaidi ya miaka 60. [1] Wanaume na wanawake wanaonekana kuathiriwa kwa uwiano sawa. [5] Pia umeripotiwa zaidi tangu miaka ya 1950. [5] [8] Kwa pamoja, ugonjwa wa uvimbe wa utumbo mkubwa na ugonjwa wa Crohn huathiri watu wapatao milioni moja nchini Marekani. [10] Kwa matibabu sahihi, hatari ya kifo inaonekana sawa na ile ya idadi ya watu kwa ujumla. [6] Maelezo ya kwanza ya ugonjwa wa vidonda vya utumbo mkubwa yalitokea karibu miaka ya 1850. [8]

Marejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 1.15 1.16 1.17 1.18 1.19 "Ulcerative Colitis". NIDDK. Septemba 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Julai 2016. Iliwekwa mnamo 3 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Runge, Marschall S.; Greganti, M. Andrew (2008). Netter's Internal Medicine E-Book (kwa Kiingereza). Elsevier Health Sciences. uk. 428. ISBN 9781437727722. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 27 Julai 2020.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Molodecky NA, Soon IS, Rabi DM, Ghali WA, Ferris M, Chernoff G, Benchimol EI, Panaccione R, Ghosh S, Barkema HW, Kaplan GG (Januari 2012). "Increasing incidence and prevalence of the inflammatory bowel diseases with time, based on systematic review". Gastroenterology. 142 (1): 46–54.e42, quiz e30. doi:10.1053/j.gastro.2011.10.001. PMID 22001864.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Wang H, Naghavi M, Allen C, Barber RM, Bhutta ZA, Carter A, na wenz. (GBD 2015 Mortality and Causes of Death Collaborators) (Oktoba 2016). "Global, regional, and national life expectancy, all-cause mortality, and cause-specific mortality for 249 causes of death, 1980–2015: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2015". Lancet. 388 (10053): 1459–1544. doi:10.1016/s0140-6736(16)31012-1. PMC 5388903. PMID 27733281.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 Ford AC, Moayyedi P, Hanauer SB (Februari 2013). "Ulcerative colitis". BMJ. 346: f432. doi:10.1136/bmj.f432. PMID 23386404.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 Wanderås MH, Moum BA, Høivik ML, Hovde Ø (Mei 2016). "Predictive factors for a severe clinical course in ulcerative colitis: Results from population-based studies". World Journal of Gastrointestinal Pharmacology and Therapeutics. 7 (2): 235–41. doi:10.4292/wjgpt.v7.i2.235. PMC 4848246. PMID 27158539.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  7. Akiho H, Yokoyama A, Abe S, Nakazono Y, Murakami M, Otsuka Y, Fukawa K, Esaki M, Niina Y, Ogino H (Novemba 2015). "Promising biological therapies for ulcerative colitis: A review of the literature". World Journal of Gastrointestinal Pathophysiology. 6 (4): 219–27. doi:10.4291/wjgp.v6.i4.219. PMC 4644886. PMID 26600980.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  8. 8.0 8.1 8.2 8.3 8.4 8.5 8.6 Danese S, Fiocchi C (Novemba 2011). "Ulcerative colitis". The New England Journal of Medicine. 365 (18): 1713–25. doi:10.1056/NEJMra1102942. PMID 22047562.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Vos T, Allen C, Arora M, Barber RM, Bhutta ZA, Brown A, na wenz. (Oktoba 2016). "Global, regional, and national incidence, prevalence, and years lived with disability for 310 diseases and injuries, 1990–2015: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2015". Lancet. 388 (10053): 1545–1602. doi:10.1016/S0140-6736(16)31678-6. PMC 5055577. PMID 27733282.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Adams, James G. (2012). Emergency Medicine E-Book: Clinical Essentials (Expert Consult – Online) (kwa Kiingereza). Elsevier Health Sciences. uk. 304. ISBN 978-1455733941. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Machi 2020. Iliwekwa mnamo 27 Julai 2020.

[[Category:Magonjwa]]